dc.description.abstract | Katika utafiti huu, mtafiti ameonyesha nafasi ya vijana kama mawakala wa kuleta mabadiliko katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea iliyotungwa na Ken Walibora mwaka wa 2012. Hii ni kutokana na rai kwamba vijana ndiyo wengi katika jamii na wanatekeleza majukumu anuwai katika jamii.Utafiti wetu uliongozwa na Nadharia ya Uyakinifu wa kijamii ambao unajihusisha na utetezi wa wanyonge na ukombozi wao. Mtafiti amebaini kwamba vijana ni mawakala wa mabadiliko na wanaweza kuleta mchango ambao unaweza kuwafaidi wanajamii wote. Hii ni kwa sababu vijana ni wenye nguvu za mwili na maarifa ambayo wanaweza kutumia ili kuifunza jamii. Mtafiti alitumia mbinu za utafiti za maktabani na mtandaoni. Maktabani, mtafiti alisoma riwaya teule na makala tofauti kama vile tasnifu, riwaya na tamthilia zingine zinazohusiana na mada pamoja na vitabu vyenye maelezo kuhusu Nadharia ya Uyakinifu wa Kijamii. Pia, alitembelea mtandao na kuangalia masuala yanayohusiana na vijana na pia alisoma maelezo kuhusu Nadharia ya Uyakinifu wa Kijamii. Utafiti huu ulibaini kuwa vijana wanatekeleza majukumu chungu nzima katika jamii kama vile kupigana na utawala mbaya na ufisadi, kupambana na tamaduni potovu, kubadili mitazamo kuwahusu walemavu, kukabiliana na wizi wa miswada na kadhalika. Masuala haya yanadhihirisha wazi kuwa vijana wana jukumu la kipekee katika kuleta mabadiliko katika jamii. | en_US |